Ankara.Wakurdi wanaotaka kujitenga washambulia. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara.Wakurdi wanaotaka kujitenga washambulia.

Duru za kijeshi nchini Uturuki zimesema kuwa wapiganaji wawili wa Kikurdi wameligonga lori lililokuwa limejazwa mafuta katika kituo cha polisi katika shambulio la kujitoa muhanga.

Baada ya mlipuko huo , wanachama wengine wa chama kilichopigwa marufuku cha Kurdistan Workers Party PKK, walishambulia kituo hicho cha polisi katika jimbo la mashariki la Tunceli.

Jeshi lilijibu shambulio hilo kwa operesheni iliyokuwa ikisaidiwa na ndege za kijeshi. Washambulizi hao wawili waliokuwa katika lori waliuwawa lakini hakuna taarifa zaidi zilizopatikana za watu waliouwawa.

Kundi hilo linalotaka kujitenga la PKK, ambalo limekuwa likipambana kutaka kujitenga tangu tangu mwaka 1984, pia lilituhumiwa kuhusika katika shambulio jingine la bomu la kujitoa muhanga mjini Ankara mwezi uliopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com