Amnesty Intl: Waandishi wa habari Somalia wanashambuliwa | Matukio ya Afrika | DW | 13.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Amnesty Intl: Waandishi wa habari Somalia wanashambuliwa

Shirika la haki za binaadamu la Amnesty International limesema leo kuwa wanahabari katika nchi yenye machafuko ya Somalia wanakumbwa na matukuo ya milipuko ya bomu, kuchapwa, kushambuliwa na kukamatwa.

Taifa hilo la Afrika Mashariki kwa muda mrefu limeonekana kuwa mojawapo ya maeneo hatari kabisa ya kufanya kazi kama mwanahabari, huku kukiwa na vitisho viwili vya kuripoti kuhusu mgogoro wa nchi hiyo na sheria kali na kandamizi zinazowekwa na maafisa. Lakini sasa, Amnesty International inasema katika ripoti yake kuwa hali inazidi kuwa mbaya. Shirika hilo la haki za binaadamu limesema ongezeko la mashambulizi ya umwagaji damu, vitisho, mateso na unyanyasaji wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, linaifanya Somalia kuwa mojawapo ya maeneo hatari zaidi duniani kwa mwanahabari. Amnesty International imeitaka serikali kuchukua hatua kukomesha ukiukaji huo. Karibu wanahabari 8 wameuawa tangu 2017, na karibu 8 zaidi wamekimbia nchi hiyo wakihofia maisha yao.