1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yamuapisha rais mpya anayepingwa na waandamanaji

19 Desemba 2019

Rais mpya wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameahidi kuanzisha ukomo wa muda wa urais, pamoja na kuwajumuisha vijana katika siasa, wakati alipojaribu kutafufa uungwaji mkono wa harakati za kudai demokrasia

https://p.dw.com/p/3V6Da
Algerien Abdelmadjid Tebboune Wahlsieger Präsidentschaftswahl
Picha: picture-alliance/AP/F. Guidoum

Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika lenye utajiri wa gesi, limemuapisha Tebboune kuwa rais hii leo. Wajumbe wa serikali ya  Algeria wanaimani kwamba, Tebboune ataisaidia nchi kurejesha utulivu baada ya miezi 10 ya maandamano ya amani lakini yenye kutishia uhalali wao na kuathiri uchumi.

Tebboune aliye na umri wa miaka 74 na ambaye ana ukaribu na kiongozi wa kijeshi aliye na nguvu nchini Algeria, amewaeleza wana vuguvugu la maandamano la Hirak kuwa katiba inatoa haki ya kuandamana.

Katika hotuba yake ya kwanza kama rais, ameahidi kushughulikia ufisadi ambao unalalamikiwa na waandamanaji na kupunguza mamlaka yake.