1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumuua mwanamke

11 Juni 2024

Bwana mmoja amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mauaji ya mwanamke mmoja aliyekuwa na ujauzito huko nchini Denmark.

https://p.dw.com/p/4gt5y
Picha ya alama | Jela
Picha yenye kuonesha gereza Copenhagen DenmarkPicha: Ritzau Scanpix/imago images

Tukio lililotokea mwaka 2016.Kwa mujibu wa mahakama ya wilaya ya Glostrup, bwana huyo mwenye umri wa miaka 30 anaelezwa kumchoma kwa kisu mwanamke huyo mara 11, na kukata kipande cha pua yake, tukio lililotokea katika bustani moja karibu na mji wa Copenhagen.Mtuhumiwa huyo alikana kosa hilo na wakili wake amesema atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Silaha ya mauaji bado haijapatikana na hakuna ushahidi wa kitaalamu kama vile alama za vidole au vinasaba (DNA) kuthibitisha hatia ya bwana huyo.