Afya na jamii | Noa Bongo | DW | 10.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Afya na jamii

Masuala ya Afya na kinga dhidi ya magonjwa yanahitaji kutiliwa mkazo hasa katika sehemu zinazokumbwa na hali duni ya maisha. Vipindi vya Noa Bongo vinatoa mfano mzuri kuhusu magonjwa hatari zaidi barani Afrika.

default

Mpango wa uzazi ni mada muhimu katika mfululizo wa vipindi vya Noa Bongo, kwani mada hii inagusia maadili ya jamii na maisha kwa jumla, njia za mpango wa uzazi na pia masuala ya kijinsia - hasa kuhusu mabadiliko ya kimawazo katika muda wa miongo ya hivi karibuni barani Afrika. Na Noa bongo pia inatambua juhudi za kutupilia mbali baadhi ya imani na tamaduni katika kupambana na magonjwa kama vile Ukimwi.

Mkazo ulitolewa katika kuimarisha juhudi za kibinafsi kukabiliana na magonjwa na pia kuimarishwa njia za kupata habari muhimu kuhusu masuala ya afya. Juhudi au mabadiliko ya kiwango chochote kile huchangia pakubwa juhudi za kuboresha maisha ya familia na jamii kwa jumla, na ndio sababu vipindi vya Noa Bongo vinalenga kukupa fursa kuwa na mtazamo na kuelekeza juhudi za kila mmoja wetu katika kuboresha afya.

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com