1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kituo cha CDC chazidisha juhudi za kinga na chanjo ya Ebola

27 Mei 2026

Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC, kimesema kuwa kimeongeza juhudi za kinga na kuharakisha maendeleo ya chanjo kufuatia mlipuko wa Ebola, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/5EOS2
DR Congo Mongbwalu 2026 | Hofu ya Ebola baada ya shambulio hospitalini
Shambulio dhidi ya hospitali huko Mongbwalu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lilisababisha wagonjwa 18 wa Ebola kukimbia, na kusababisha.Picha: DW

Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC, kimesema kuwa kimeongeza juhudi za kinga na kuharakisha maendeleo ya chanjo kufuatia mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Jean Kaseya, alisema siku ya Jumanne kuwa hatua hizo mpya zinachukuliwa ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo na kuzuia athari zake kuongezeka katika ukanda huo.

"Kwa sasa tunachokifanya ni kuharakisha chanjo. Afrika CDC ni sehemu ya timu inayofanyia kazi utengenezaji wa chanjo. Wakati huo tunaendelea kutekeleza yale tuliyojifunza kutoka milipuko iliyopita ya Ebola. Hii inamaanisha kutumia hatua za afya ya umma ili kukomesha maambukizi," alisema mkurugenzi wa CDC.

Wakati huo huo, wahudumu wa misaada ya kiutu na wataalamu wa afya, wamesema kwamba ukosefu wa miundombinu ya huduma za afya, kunaendelea kudhoofisha juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola nchini Kongo.