1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Afisa wa juu wa kundi la Kiislamu, Palestina afariki jela

Saumu Mwasimba
2 Mei 2023

Kifo cha mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kiislamu la Palestina la vuvuguvu la Jihad kilichotokea akiwa chini ya ulinzi wa Israel,kimezusha ghadhabu kubwa miongoni mwa viongozi wa Palestina.

https://p.dw.com/p/4Qo2h
Trauer um Khader Adnan, einem palästinensischen Gefangenen, der im israelischen Gefängnis starb
Picha: Majdi Mohammed/AP

Khader Adnan mwenye umri wa miaka 44 alikutwa amepoteza fahamu akiwa seli ya jela alikokuwa akizuiliwa leo asubuhi kwa mujibu wa msemaji wa magereza,na zilifanyika juhudi za kumuokoa na kukimbizwa hospitali lakini alifariki.

Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh ameishutumu Israel kwa kile alichokiita mauaji ya makusudi ya Adnan kwa kumkatalia ombi lake la kutaka kuachiliwa,kupuuza kumpa matibabu na kumuweka seli licha ya hali yake ya kiafya.

Wizara ya mambo ya nje pia imeitwisha dhamana Israel kwa kifo cha Mpalestina huyo.Jeshi la Israel limesema kiasi maroketi 22 yamefyetuliwa kuelekea miji kadhaa ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza.

Adnan alikuwa akiendesha mgomo wa kususia kula kwa kiasi miezi mitatu tangu Februri 5 na alikuwa akishikiliwa jela kwa kosa la kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na kuunga mkono ugaidi na uchochezi.