AFCON 2013: Umdhanie sie kumbe ndie | Michezo | DW | 23.01.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

AFCON 2013: Umdhanie sie kumbe ndie

Michezo ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2013,ilitawaliwa kabla ya kuanza na mazungumzo mitaani kuhusu tembo wa Cote D'Ivoire,timu ya taifa ya Cote D'Ivore na mchezaji wao nyota Didier Drogba.

Members of the public pose for photographs and check out the new Africa Cup Of Nations ( AFCON ) sign set up in Dr Yusuf Dadoo Street in Durban on January 15,2013 welcoming the Africa Cup of Nations visitors to the city of Durban. The signs are to publicise the hosting of the 2013 AFCON Cup Football tournament taking place in South Africa.The organisers have been critiised for the late publicity on promoting the AFCON tournament.Durban is one of the host cities and Bafana Bafana open the tournament against the Cape Verde on January 19,2013. AFP PHOTO / RAJESH JANTILAL (Photo credit should read RAJESH JANTILAL/AFP/Getty Images) Erstellt am: 15 Jan 2013

AFCON 2013

Lakini Congo na Ethiopia zilikuja kutawala mazungumzo hayo kutokana na ujasiri walioonesha katika mashindano hayo.

Chui wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo waliweka kando manung'uniko yao kuhusu fedha za bonasi pamoja na unyanyasaji wanaotendewa na maafisa wa timu hiyo na kufuta kipigo cha mabao 2-0 na hatimaye kumaliza mchezo wao dhidi ya Ghana kwa sare ya mabao 2-2.

Democratic Republic of Congo players pose for a team photo ahead of their World Cup 2014 Africa Zone qualifying match against Togo in Kisnhasa on June 10, 2012. AFP PHOTO/JUNIOR D.KANNAH (Photo credit should read JUNIOR D.KANNAH/AFP/GettyImages)

Kikosi cha Chui wa Kongo

Ghana ilipewa nafasi ya juu

Ghana waliwekwa katika nafasi ya juu na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo mwishoni kabisa katika kundi B na mchezo wao uliofanyika mjini Port Elizabeth ulionekana kuwa unakwenda katika mwelekeo wa utabiri huo, wakati Emmanuel Agyeman Badu na Kwadwo Asamoah walipopachika mabao ya Black Stars wa Ghana.

FIFA WORLD CUP 2010 TEAMS Picture taken 15 November 2009 of team Ghana prior to the FIFA World Cup 2010 qualification match against Mali in Kumasi, Ghana. Back from left: Richard Kingston, John Pantsil, Eric Addo, Jonathan Quartey, Asamoah Gyan, Stephan Appiah. Front from left: Michael Essien, Anthony Annan, Matthew Amoah, Samuel Inkoom, Sulley Muntari. Ghana is among the 32 teams that qualified for the FIFA World Cup 2010. EPA/JANE HAHN

Black Stars ya Ghana

Lakini Chui hao wa msitu wa Virunga hawatabiriki na badala ya kusalimu amri, walifanikiwa kupata mabao mawili kutoka kwa nahodha wao, Tresor Mputu, na Dieumerci Mbokani alisawazisha kwa mkwaju wa penalti.

Mali inashikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa kundi B baada ya kuwalazimisha Niger kuacha ubishi zikiwa zimesalia dakika sita kabla mchezo kumalizika wakati golikipa, Daouda Kassaly, kujikuta hana hakika ya kuukamata mpira wa juu na kumzawadia Seydou Keita fursa adimu ya kupachika bao.

Ethiopia yarejea kwa kishindo

Ethiopia, ikirejea katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa ya Afrika baada ya ukame wa miaka 31, ilikosa penalti, na mlinda mlango wao Jemal Tassew alitolewa nje kwa kadi nyekundu na wakafungwa bao na mabingwa watetezi Zambia kabla ya kwenda mapumziko katika uwanja wa Nelspruit.

epa03092408 Kennedy Mweene of Zambia celebrates his team first goal during the Africa Cup of Nations match between Zambia and Sudan in Bata, Equatorial Guinea, 04 February 2012. EPA/STR EDITORIAL USE ONLY +++(c) dpa - Bildfunk+++

Golikipa wa Chipolopolo Kennedy Mweene

Lakini paa hao wa Walias walinakili yale yaliyofanywa na Chui wa Congo na kuweza kusawazisha bao hilo kwa gonga safi na kuuweka mpira wavuni wakimwacha golikipa wa Chipolopolo, Kennedy Mweene, akigaaga chini.

Burkina Faso na Nigeria nazo zina pointi moja kila mmoja katika kundi C

Didier Drogba jubelt nach dem Sieg der Elfenbeinküste über Nigeria beim Afrika-Cup (Archivfoto vom 07.02.2006). Die «Elefanten», die ivorische Nationalmannschaft, hat sich zum ersten Mal für die Weltmeisterschaft qualifiziert. Immer wenn die«Elefanten» spielen, wie zuletzt beim Afrika-Cup, dann ist die Stadt Abidjan so gut wie ausgestorben. Foto: Adrian de Kock dpa (zu dpa-Serie Länderporträts Nur Fußball eint unser Land - Elfenbeinküste freut sich auf die WM vom 14.02.2006) +++(c) dpa - Bildfunk+++

nahodha wa Cote D'Ivoire Didier Drogba

. Togo iliwashangaza watabiri kwa kuiita timu isiyokuwa na matumaini katika timu 16 zilizofikia fainali, na ilibakisha tu dakika mbili kabla ya kuikaba koo Cote D'Ivoire katika kundi D, pale iliposalimu amri dakika za majeruhi na kukubali kipigo cha mabao 2-1. Lakini hata hivyo ilionyesha kandanda la ujasiri.

Leo ni zamu ya wenyeji Bafana Bafana, Afrika kusini kuonesha kuwa ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kutoroka na taji hilo, wakati itakapopambana na Angola. Wageni wa mashindano haya, Cape Verde, wakiwa katika hali sasa ya kujiamini wanatiana kifuani na Morocco.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Josephat Charo