Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May leo ameahidi kuliruhusu Bunge kuchelewesha mchakato wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya maarufu Brexit kwa hadi miezi mitatu// Urusi imeelezea wasiwasi wake kwamba Marekani inajiandaa kuiingilia Venezuela kijeshi// Watu 57 waliokuwa wapiganaji wa kundi la M23 waliokimbilia Uganda wamerudishwa kwa hiari yao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.