1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Vyombo vya habari

Ipokee DW kupitia RSS

5 Februari 2012

Viungo vya RSS vinakusaidia kujisajili au kusoma ukurasa wa wavuti au makala kwenye tovuti. Taarifa huhamishiwa mara moja kwenye kompyuta yako au kifaa chochote kingine unachotumia.

https://p.dw.com/p/13wE9
02_2012 Themenbild für RSS
Themenbild RSS

RSS ina maana ya "Really Simple Syndication" na mara nyingi hutambuliwa kama kiungo cha RSS. Kiungo cha RSS hutumiwa kupeleka ujumbe au maelezo mafupi ya makala kwenye tovuti au kitu kingine chochote kinachotangazwa.

Faida za teknolojia hii ya kiungo cha RSS

RSS huwawezesha wanaoitumiakujisajili kwenye ukurasa wa wavuti au sehemu ya ukurasa wa wavuti. Unaweza kuhamishia habari zinazohusika kwenye kompyuta au kifaa chochote kingine.

Kiungo hiki huwawezesha wanaokitumia kupata taarifa za karibu na za kisasa mara moja na kwa njia rahisi. Teknolojia hii hutumika kwenye maandishi na pia mada zenye vielelezo vya sauti na video.

Pata kiungo cha RSS bure (bila malipo)

DW katika mitandao ya kijamii
DW katika mitandao ya kijamii

Kujisajili kwenye kiungo cha RSS unatakiwa kupata kiungo cha kusoma data. Kiungo hicho kitarekebisha upya mada ulizojisajili pindi unapofungua. Viungo kama My Yahoo, Bloglines na Newsgator vinakuwezesha kupata, kusoma na kurekebisha data zako kwenye kompyuta iliyounganishwa na tovuti.

Viungo vingi vya mifumo ya kusoma data vinapatikana bure kwenye tovuti. Kwa taarifa zaidi tizama

http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_feed_aggregators

Mtandao wako binafsi wa tovuti.

Ni rahisi sana kutumia viungo vya tovuti. Unapotaka kujisajili kwa kiungo fulani kwenye ukurasa wa wavuti nakili na upachike anwani yako ya tovuti kwenye mfumo wako wa kusoma tovuti. Mifumo mipya ya tovuti kama vile Firefox, Safari na Internet Explorer inakuwezesha kufanya hayo moja kwa moja.

Mifumo hii mipya huchunguza iwapo kuna viungo vya tovuti kwenye kila ukurasa wa wavuti unaofungua. Iwapo kuna viungo vipya, mfumo huo utaonyesha taswira ya RSS kwenye kisanduku cha anwani.

Mada za ukurasa wako wa wavuti

Unaweza kuvitumia viungo vya tovuti kwa matumizi yako binafsi na pia unaweza kuvitumia kuonyesha mada au taarifa za kurasa nyingine za wavuti kwenye wavuti au blogu yako.

DW.DE pia inakupa huduma ya kisanduku cha kuweka taarifa kwenye ukurasa wako wa wavuti. Unaweza kuandaa kisanduku hicho kujumuisha taarifa zote unazotaka kutoka ukurasa wa habari wa DW.DE.

Kwa kutumia mfumo huu wa viungo, taarifa za karibuni zinahamishwa moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa wavuti bila ya kuhitajika kuhariri au kuandika upya taarifa hizo. Huduma hii inakuunganisha na watumizi wapya.

Masharti ya kutumia

Tafadhali fahamu ya kwamba maudhui ya taarifa hayabadilishwi kwa njia yoyote ile. Taarifa hizo ni lazima ziandamane na nembo ya asili yake yaani DW.DE. Matini ya asili lazima iunganishwe na wavuti wa DW.DE. Taarifa hizo zisipelekewe kwa mtu au asasi nyingine.

Unaruhusiwa kutumia taarifa hizo kwenye ukurasa wako lakini huruhusiwi kuzihifadhi. Haki ya kutumia taarifa zetu si za kipekee.

Tafadhali wasiliana nasi!

Huduma yetu ya habari hutolewa kwa mtindo wa XML (RSS) au kama kisanduku cha vidokezo kinachoweza kujumuishwa kwenye ukurasa wako kwa kutumia JavaScript. Viunzi hivyo vinajumuisha kichwa cha habari na vidokezo pamoja na taarifa za kusikiliza na kanda za video.

Kama unataka, tafadhali wasiliana nasi kupitia

bildung@dw.de na ujumuishe taarifa ifuatayo kwenye barua-pepe yako:

  • Jina la ukurasa wa Wavuti
  • Jina la mtu wa kuwasiliana naye
  • Mada unazotaka