Islamabad.Mushara ahalalisha mauaji yaliyofanywa na helikopta za kijeshi. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Islamabad.Mushara ahalalisha mauaji yaliyofanywa na helikopta za kijeshi.

Rais wa Pakistan Pervez Musharaf amesema kuwa watu 80 waliouwawa katika mashambulizi ya helikopta za kijeshi katika shule ya kidini kaskazini- magharibi mwa nchi yake karibu na mpaka na Afghanistan, kwamba wote walikuwa ni wanamgambo waliokuwa wakipewa mafunzo.

Tangazo hilo limekuja baada ya maelfu ya waandamanaji kuingia mitaani karibu na mji wa Khar wakiandamana kupinga mashambulizi hayo ya anga.

Maafisa wa kijeshi wa Pakistan wamesema, walifanya mashambulizi hayo baada ya kupata taarifa kutoka kwa makachero wa Marekani.

Kiongozi wa Wataliban katika eneo hilo anasemekana anawahifadhi wanamgambo katika shule hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com