1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wellington:Meli ya Kijapani ya kuvua nyangumi na ambayo imeharibika katika eneo la Antarktis bado haijaweza kujikwamua kutoka kwenye barafu na theluji.

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR0

Jumuiya ya ulinzi wa mazingira ya Green Peace imesema mabaharia katika meli hiyo hawajafaulu kuifanya injini ya meli hiyo ifanye kazi tena. Meli hiyo, kwa jina Nisshin Maru, kutokana na amari ya serekali ya Japan, hadi sasa imelikataa ombo la kuvutwa. Kikosi cha uokozi cha New Zealand, nchi ambayo ndio yenye dhamana katika eneo hilo, kimeitaka meli hiyo iondoke kwa haraka kama iwezekanavyo kutoka eneo hilo tete la Ozone. Kwa vile hali ya hewa inazidi kuwa mbaya kuna hatari kwamba sehemu ya tani alfu moja ya mafuta na kemikali ziliomo ndani ya meli hiyo itamwagika baharini na kusababisha maafa ya kimazingira.