1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhamisho na Usajili Ujerumani

22 Julai 2011

Wakati shughuli za uhamisho na usajili wa wachezaji ukiendelea katika matayarisho ya kuanza msimu nchini Ujerumani, timu ya Werder Bremen inakosa kushiriki katika hili kabla ya kuanza msimu huo mpya

https://p.dw.com/p/121wi
Claudio Pizarro wa timu ya Werder BremenPicha: picture alliance/Pressefoto Ulmer

Timu ya Werder Bremen inakosa kushiriki katika hili kabla ya kuanza msimu huo mpya, na ni kutokana na kuwa hawajapata wafadhili wapya na hawajafanikiwa kuuza wachezaji wowote.

Trainingsauftakt Werder Bremen
Denni Avdic (kati) Said Husejinovic (kushoto) Per Mertesacker wa Werder BremenPicha: picture alliance/dpa

Mwenyekiti wa bodi ya usimamizi ya timu ya Werder Bremen, Willi Lemke, amesema timu hiyo ambayo imeshindwa kufuzu kwa mashindano ya kuwania ubingwa wa Ulaya na pia ligi ya Ulaya, inahitaji kuhifadhi fedha .

Na inaweza kuingia katika masoko ya uhamisho tu kwa kufanikiwa kuwauza wachezaji wake au kwa kupata mfadhili mpya.

Bajeti ya timu hiyo ilipungua kwa kiwango kikubwa kwa kushindwa timu hiyo kwenye mashindano ya Ulaya. Katika misimu ya awali, timu hiyo ilifanikiwa kwa ushindi kwenye mashindano hayo, ni pia kutokana na kuweza kuwauza wachezaji wake kama vile wa kiungo cha kati, Mesut Özil, kwa timu ya Real Madrid ya Uhispania na pia Mbrazil, Diego, kwa timu ya Juventus.

Deutschland Fußball Werder Bremen Mesut Özil wechselt zu Real Madrid
Mesut Özil alipokuwa akiichezea Werder BremenPicha: AP

Kwengineko Mchezaji wa zamani wa soka nchini Ujerumani, Rene Schnitzler, amepigwa marufuku ya miaka miwili na nusu kushughulika kwa njia yoyote na mchezo wa soka, baada ya kukiri kupokea pesa kupanga matokeo ya mechi za divisheni ya pili mnamo mwaka 2008.

Schnitzler alikuwa akiichezea timu ya St.Pauli wakati huo na alishuka kwenye soka ya kieneo alipojitoa kwenye timu hiyo mwaka mmoja baadaye.

Kashfa za upangaji matokeo ya mechi kwa mara nyingi ukihusisha kamari, imezusha wasiwasi mkubwa katika mchezo wa kandanda katika miaka ya hivi karibuni . Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, linachunguza mechi 29,000 kila mwaka kutafuta makosa yoyote au dalili zozote za kamari na hupokea taarifa kutoa kampuni 400 za kamari.

Schnitzler alikiri kupokea Euro laki moja kutoka kwa wawakilishi Wakiholanzi wa kampuni ya kamari kushawishi michezo na kuwa aliathirika katika kamari tangu akiwa na umri wa miaka 18.

Vyombo vya habari Ujerumani vinasema mechi hizo zilizopangwa zilkuwa dhidi ya timu kama Hansa Rostock, Duisburg, Augsburg na mara mbili dhidi ya Mainz.

Ama kwengineko katika mchezo wa masumbwi barani Afrika.

Matokeo mabaya ya wanamisumbwi wa Afrika kusini katika mashindano ya jumuiya ya madola nchini India yamesababisha wakuu wa mchezo huo Afrika kusini kuwatuma wapiganaji 10 bora wa mchezo huo nchini Cuba katika jitihada za kuepusha kushindwa namna hiyo katika mashindano ya mwakani ya Olimpiki mjini London, Uingereza.

Bildgalerie Jahresrückblick 2008 Oktober Deutschland
Picha: AP

Wanamisumbwi 4 walioshiriki mashindano hayo ya New Delhi walishindwa sio tu kujinyakulia mataji, bali pia kushinda hata pigano moja. Na kuendeleza kuishukisha rekodi ya nchi hiyo ambayo tangu iruhusiwe kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa haijapata washindi wa medali yoyote.

Katika wiki zinazokuja, kundi la wanamisumbwi hao wa Afrika kusini watajifunza mbinu ambazo zimeifanikisha Cuba kuwa ngome kuu ya mashindano hayo katika kiwango cha Olimpiki.

Mojawapo ya wanamisumbwi hao amesema wana matumaini ya kijufunza mengi, maana ni kama kuwatuma wachezaji soka nchini Brazil ambayo inatambulika kuwa ngome ya mchezo huo. Cuba ni mojawapo ya mataifa makuu ya uchezaji masumbwi, na imeongoza katika mashindano ya Olimpiki, ikijishindia medali 32 za dhahabu tangu mwaka 1968 na imekuwa na uhusiano mzuri na Afrika Kusini tangu enzi za kupinga ubaguzi wa rangi.

Licha ya kuwa masumbwi ni mchezo maarufu nchini Afrika kusini, nchi hiyo haijawahi kushinda medali zozote tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1992.

Mwandishi Maryam Abdalla/Afpe/Dpae
Mhariri: Miraji Othman