Taasisi za utafiti za Ulaya na Marekani zakata mawasiliano na Taasisi ya taaluma za siasa na uhusiano wa kimataifa huko Iran. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Taasisi za utafiti za Ulaya na Marekani zakata mawasiliano na Taasisi ya taaluma za siasa na uhusiano wa kimataifa huko Iran.

Tehran:

Karibu ya taasisi za utafiti 40 za Ulaya na Marekani zimesema zitasimamisha mawasiliano na taasisi maarufu ya utafiti katika Iran ambayo ilisaidia kuandaa nchini humo mkutano wa wiki iliopita uliohudhuriwa na watu wanaokana juu ya kutokea mauaji ya kiholela ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Taasisi hizo zimekubali kusitisha programu zinazoendelea sasa pamoja na taasisi ya Iran juu ya taaluma za siasa na uhusiano wa kimataifa. Mkutano huo uliofanywa wiki iliopita uliwakusanya watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaokana juu ya kutokea mauaji ya kiholela dhidi ya Wayahudi. Watu hao walijadiliana kama mauaji hayo yalifanyika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com