1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Sydney.Howard atamka wazi kuwa hajutii Australia kuungana na Marekani katika vita dhidi ya Iraq.

Waziri mkuu wa Australia John Howard amesema, hajutii hata kidogo kuungana na jeshi linaloongozwa na Marekani katika vita vya Iraq, licha ya uongozi wa rais Bush kushindwa katika uchaguzi baraza la Congress.

Howard ambae serikali yake inakabiliwa na uchaguzi baadae mwakani amesema, raia wengi wa Australia wataunga mkono kuondoshwa kwa vikosi vya kijeshi nchini Iraq, hata kama hawakuunga mkono hapo awali kushiriki kwa uvamizi huo mwaka 2003.

Amesema wananchi wengi wataunga mkono vikosi vya wanajeshi wa Australia vibakie nchini Iraq hata kama hawakuunga mkono hapo awali kujiunga kwao na nchi shirika mwaka 2003.

Akizungumza kupitia radio ya kibiashara, waziri mkuu John Howard amesema haamini kama Wa-Australia watataka wanajeshi wao watoke kwa pupa namna hiyo.

Nchi ya Australi ina jumla ya wanajeshi 1,400 nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com