ROME:mjumbe mpya wa Iran bado ashindikizwa na Larijani mjini Rome | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROME:mjumbe mpya wa Iran bado ashindikizwa na Larijani mjini Rome

Mjumbe mpya wa Iran juu ya suala la nyuklia la nchi hiyo leo anaingia katika jukwaa la kimataifa mjini Rome kwa mara ya kwanza, ambapo atashiriki kwenye mazungumzo yatakayozipa fursa nchi za magharibi kubaini iwapo Iran imezidi kuwa na msimamo mkali juu ya mpango wake wa nyuklia.

Mjumbe huyo mpya bwana Saeed Jalili anatazamiwa kukutana na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana.

Bwana Jalili ataongozana na mjumbe wa hapo awali bwana Ali Larijani alietangaza kujiuzulu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com