1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH: Iran na Saudi Arabia kujadili hali ya Mashariki ya Kati

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran hii leo anaanza ziara yake ya siku mbili nchini Saudi Arabia.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Tehran,azma ya ziara hii rasmi ya kwanza ya Ahmedinejad kukutana na viongozi wa Saudi Arabia,ni kujadili hali ya Mashariki ya Kati.Wadadisi wa kisiasa wameshangazwa na ziara hii kwa sababu inafahamika kuwa kimkakati Saudi Arabia ni mshirika wa Marekani.Vile vile Saudi Arabia na Iran zipo pande mbali mbali kuhusu migogoro ya umwagaji damu,kati ya Wasunni na Washia nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com