Rais Mahamoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi yake haihitaji kuwa na silaha za nuklia na kwamba haina mpango wa kuingia vitani na Marekani. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Mahamoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi yake haihitaji kuwa na silaha za nuklia na kwamba haina mpango wa kuingia vitani na Marekani.

Akizungumza katika mahojino na kituo cha televisheni cha Marekani mjini Teheran kabla ya kueleka New York katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais huyo wa Iran amesema kuwa ni makosa kufikiria kuwa Marekani na Iran zinajianda kuingia vitani.

Rais Ahmednejad anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kesho, katika hotuba inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Matamshi hayo ya rais wa Iran yanakuja siku moja tu baada ya kuonya kuwa yoyote atakayejaribu kuishambulia Iran, atajutia uamuzi wake, ijapokuwa alisema kuwa jeshi la nchi hiyo ni kwa ajili ya kujilinda.

Rais huyo wa Iran leo hii anatarajiwa kutoa mhadhara katika chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com