Nchini Kongo Rais Joseph Kabila amekutana mjini Kinshasa na mabalozi wa nchi 5 wanachama wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuwahamasisha kuhusu operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa FDLR
Operesheni hizo zinaendeshwa kwa pamoja na jeshi la Kongo na lile la Rwanda.Wakati huohuo Spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Vital Kamere ameshutumu vikali kualikwa kwa wanajeshi wa Rwanda nchini mwake.Wanajeshi hao wa Rwanda waliingia mashariki mwa Kongo mnamo siku ya Jumatatu.
Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa katuletea ripoti ifuatayo.