Wasiwasi katika zoezi la kutaka kuwavuwa silaha kwa nguvu huko Kongo wapiganaji wa Chama cha FDLR cha Rwanda
14 Januari 2009Matangazo
Baadhi ya wananchi wa huko Mashariki mwa Kongo wameelezea wasiwasi kuhusu operesheni iliokusudiwa kufanywa ya kuwalazimisha waasi wa Kinyarwanda wa Chama cha FDLR wanaojihifadhi katika eneo hilo kuvuliwa silaha. Wasiwasi huo pia ulielezwa kwenye kiwanja cha ndege cha Goma alipowasili mjini humo waziri wa mambo ya ndani wa serekali kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Selestin Mbuyu. Mwandishi wetu wa huko Goma, John Kanyunyu, ametutumai ripoti ifuatayo: