1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni misaada ipi ya kijeshi Marekani inaipatia Israel?

9 Aprili 2024

Kuzuiliwa kuingia kwa misaada ya kiutu katika ukanda wa gaza kumepelekea kutolewa mwito kwa Marekani wa kuweka masharti ya mabilioni ya dola katika ufadhili wake wa kijeshi na misaada mingine inayotoa kwa Israel

https://p.dw.com/p/4eYTl
Gaza Israel
Wanajeshi wa Israel wakiwa katika operesheni katika ukanda wa GazaPicha: Israeli Army/Handout/AFP

 
Kuzuiliwa kuingia kwa misaada ya kiutu katika ukanda wa gaza kumepelekea kutolewa mwito kwa Marekani wa kuweka masharti ya mabilioni ya dola katika ufadhili wake wa kijeshi na misaada mingine inayotoa kwa Israeli, ambayo imepokea zaidi msaada kutoka kwa Marekani tangu Vita vya Pili vya Dunia kuliko nchi nyingine yoyote.

Mwaka 2016, serikali ya Marekani na Israeli zilitia saini ya tatu ya Mkataba wa Makubaliano wa miaka 10, unaohusu kipindi cha kuanzia tarehe 1 Oktoba 2018 hadi Septemba 30, 2028. Mkataba huo wa makubaliano unatoa jumla ya Dola bilioni 38 za Kimarekani kama msaada wa kijeshi katika kipindi cha miaka 10, dola bilioni 33 za ruzuku kwa ajili ya kununua vifaa vya kijeshi na dola bilioni 5 kwa ulinzi wa mifumo ya makombora.

Israel inapata mifumo gani ya silaha za kisasa?

Israel ni nchi ya kwanza duniani kuwa na ndege za kivita aina ya F-35 zinazotajwa kuwa ni ndege zenye ubora mkubwa zaidi wa kiteknolojia kuwahi kutengenezwa duniani. Israel iko pia katika mchakato wa kununua ndege 75 za kivita chapa F-35 na hadi mwaka uliopita tayari nchi hiyo ilikuwa imepokea ndege hizo 36 ilizozinunua kwa msaada wa marekani.

Soma zaidi. Netanyahu asema Israel iko karibu kushinda vita vyake dhidi ya Hamas

Marekani pia imeisaidia Israel kuendeleza na kuipatia  mifumo ya ulinzi ya Irone Dome ya kuzuia  mashambulizi ya roketi za  masafa mafupi. Mfumo huo ulitengenezwa baada ya
Vita vya 2006 kati ya Israel na Kundi la Hezbollah la nchini Lebanon.Marekani imetuma mara chungu nzima mamilioni ya dola kuisaidia Israel .

GAZA/ Israel
Picha: Gil Cohen Magen/Xinhua News Agency/picture alliance

Marekani pia imesaidia kufadhili mfumo wa "David's Sling"ulioundwa ili kurusha roketi zinazorushwa kutoka kilomita 100 hadi kilomita 200.

Je, Isreal itaendelea kupata misaada zaidi kwa kuzingatia kampeni yake dhidi ya HAMAS?

Mwaka uliopita, Rais Joe Biden aliliomba  bunge kuidhinisha 
Muswada wa matumizi ya ziada wa Dola bilioni 95 ambayo itajumuisha bilioni 14 kwa Israel pamoja na dola zingine bilioni 60 kwa Ukraine, msaada kwaTaiwan na mabilioni ya misaada mingine ya kiutu.

Soma zaidi. Guterres ataka uchunguzi huru vifo vya watoa misaada Gaza

Kifurushi hicho kilipitishwa na baraza la seneti kwa asilimia 70 mwezi Februari mwaka huu lakini muswada huo umezuiliwa katika bunge la Marekani, pingamizi ambalo viongozi wa chama cha Republican hawatoupigia kura kwa sababu ya pingamizi lao la fedha zaidi kwa ajili ya Ukraine.

Pingamizi hilo hilo linapingwa pia na baadhi ya wanachama wa Demokrat wanaoegemea mrengo wa kushoto ambao wanapinga kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza amabayo imeua zaidi ya watu 30,000.

Ni misaada  ipi mingine ambayo Marekani inatoa kwa Israel?

Israel | Gaza
Vifaa vya kijeshi vya Israel Picha: Ohad Zwigenberg/AP/dpa/picture alliance

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikitumia kura yake ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia maazimio yanayoonekana kuikosoa Israeli. Mapema wakati vita huko Gaza vilipozuka Marekani ilipiga kura ya turufu kwenye hatua zilizojumuisha wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano.

Soma zaidi. Israel yakabiliwa na shinikizo kubwa kuhusu vita vyake Gaza

Ili azimio liweze kupitishwa katika Baraza la Usalama, azimio linahitaji angalau kura tisa za kuunga mkono na ikiwa hakuna kura ya turufu ya Marekani, Ufaransa, Uingereza,Urusi au Uchina.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Marekani iliacha utamaduni wake wa kuikingia kifua Israel kwa kutokupiga kura juu ya azimio la kutaka kusitisha mapigano.

Kwa upande mwigine kutokupiga kura kwa Marekani kwenye baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kulitafsiriwi kuiunga mkono Israel katika kupinga matumizi yake ya kijeshi kwa wapelestina.