1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania kuitambua Palestina kama taifa huru

2 Aprili 2024

Uhispania imetangaza kuwa itaitambua Palestina kama taifa huru kufikia mwezi Julai mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4eL6G
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.Picha: Oscar del Pozo/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pedro Sanchez kabla ya kuanza hapo jana ziara yake Mashariki ya Kati ambako atayatembelea mataifa ya Jordan, Qatar na Saudi Arabia.

Kauli hiyo isiyo rasmi ya Sanchez ilinukuliwa na vyombo vya habari vya Uhispania ikiwa ni pamoja na shirika la habari la serikali (EFE) na magazeti El Pais na La Vanguardia, na ilieleza kuwa hivi karibuni kunatarajiwa msukumo kutoka nchi mbalimbali za Ulaya ili kuchukua msimamo kama huo.

Soma zaidi:Shinikizo lachochea baraza jipya la mawaziri Palestina kutangazwa 

Mwezi Novemba mwaka jana, nchi za Kiarabu na zile za Umoja wa Ulaya zilikubaliana katika mkutano wao huko Uhispania kwamba suluhisho la mataifa mawili ndilo jibu kwa mzozo wa Palestina na Israel.

Tangu mwaka 1988, jumla ya nchi 139 kati ya 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa tayari zimeitambua Palestina kama taifa huru.