1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Guterres ataka uchunguzi huru vifo vya watoa misaada Gaza

6 Aprili 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru kwa vifo vyote vya wafanyakazi 196 wa misaada ya kiutu waliouawa kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eURl
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Omar Havana/AP/picture alliance

Mwito wa mwanadiplomasia huyo mkuu wa ulimwengu unakuja wakati viongozi duniani wanaongeza mbinyo dhidi ya Israel kufuatia shambulizi la jeshi la Israel lililosababisha vifo vya wafanyakazi 7 wa kutoa misaada mapema wiki hii.

Hapo jana Ijumaa Jeshi la Israel lilikiri kufanya makosa makubwa yaliyopelekea vifo vya watumishi hao wa shirika la hisani la World Central Kitchen.

Mataifa mengi ikiwemo Uingereza na Poland ambazo zimepoteza raia wake kwenye mkasa huo yanataka uchunguzi huru ufanyike kubaini kile kilichotokea.

Miito pia imeongezeka ya kuitaka Israel iruhusu msaada zaidi wa kiutu kuingia Gaza. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani

Annalena Baerbock amesema hakuna tena sababu ya kuchelewesha misaada kuingia Gaza baada ya miezi sita ya vita.