1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.Hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa inategemewa kuendelea na kura juu Venezuela na Guatemala.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1t

Venezuela na Guatemala hii leo zinapanga kuanza upya juhudi za kupata kiti kisicho cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hali hiyo imekuja baada ya kushindwa mizunguuko 10 ya upigaji kura katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa, kufuatia nchi hizo kukosa thuluthi mbili ya uungwaji mkono inayohitajika.

Chini ya sheria za Umoja waMataifa, upigaji kura unaweza ukaendelea.

Kwa upande wa mataifa mengine, Afrika ya Kusini, Indonesia, Italy na Belgium zimefanikiwa kushinda wingi wa kura unaohitajika ili kuwa na kiti kisicho cha kudumu kwa kipindi cha miaka miwili katika baraza hilo la usalama, kuanzia tarehe Mosi, January mwakani.