1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndugu wawili wakutana baada ya miaka 40

23 Desemba 2016

Ndugu wawili wakutana katika kituo cha kuwatunza wazee, baada ya kupoteana kwa zaidi ya miaka 40. Unaapoisikia habari hii kwanza utafikiri imetungwa makusudi wakati huu wa X-Mas kwa jinsi inavyosisimua

https://p.dw.com/p/2UmyF
Deutschland Zwei Schwestern finden sich nach 40 Jahren im Altersheim wieder
Ndugu wawili wakutana baada ya miaka 40 katika nyumba ya wazeePicha: picture-alliance/dpa/R. Priebe

Ndugu wawili wakutana katika kituo cha kuwatunza wazee, baada ya kupoteana kwa zaidi ya miaka 40. Unaapoisikia habari hii kwanza utafikiri imetungwa makusudi wakati huu wa X-Mas kwa jinsi inavyosisimua. Lakini si hadithi ya kubuni ni tukio la kweli tena lililotokea Desemba sita iliyopita-wenyewe Ujerumani wanaiita siku hiyo kuwa ni siku ya Nikolaus. Siku hiyo ya Desemba sita mnamo saa za usiku, Hedwig Horsch amekaa mwenyewe pamoja na wazee wenzake katika meza wakisubiri chakula cha usiku-mbele yake kulikuwa na bibi mmoja. Macho ya Hedwig hayakutulia yalimwandama bibi yule ambae ni mpya katika kituo chao cha akuwatunza wazee. Hedwig hakuweza tena kuvumilia, akapiga moyo konde na kumwendeya yule bibi na kumuuliza anaitwa nani. Hapo hajawa na shaka yoyote: Mbele yake ameketi dadaake, Annelore ambae alifikiri amepotea-walionana kwa mara ya mwisho miaka 40 iliyopita. Kwa muendelezo wa kisa hiki, Msikilize Sudi Mnette katika kipindi karibuni Jumamosi saa 12:30 Jioni.