1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Harakati za polisi kupambana na Mungiki

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpR

Matumizi ya nguvu yaliyoandamana na mauaji, yameongezeka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi,wakiuawa kiasi ya watu 20,mkesha wa kuamkia leo.Polisi imesema,watu hao ni pamoja na 2 waliokutwa wamekatwa vichwa na wengine 17 kuuawa katika mapigano ya risasi na polisi.

Mauaji hayo yametokea katika eneo la Banana Hill,nje ya mji wa Nairobi.Polisi wamekuwa katika harakati za kupambana na kundi la Mungiki, linaloshukiwa kuhusika na baadhi ya mauaji au mauaji yote yaliotokea jana usiku.Umwagaji damu huo,umezusha wasiwasi kwamba wafuasi wa Mungiki, wamekusudia kuvuruga uchaguzi mkuu ujao, unaotarajiwa kufanywa mwezi wa Desemba.Kundi hilo,lina maelfu ya wafuasi,wote wakiwa ni kutoka kabila la Kikuyu,lililo kubwa nchini Kenya.