NAIROBI: Eritrea yakosolewa na Umoja wa Mataifa | Habari za Ulimwengu | DW | 26.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Eritrea yakosolewa na Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa umesema Eritrea imelipelekea kwa siri kiwango kikubwa cha silaha kundi la wanamgambo wa kisomali lililo na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Eritrea imefanya hivyo kinyume na marufuku ya kimataifa ya kuizuia silaha Somalia na kupelekwa kwa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kwenye ripoti yao iliyowasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa miongoni mwa silaha zilizo mikononi mwa wanamgambo hao wa kisomali wanojiita kwa jina Shabab, ni makombora, mikanda ya mabomu inayotumiwa na watu wa kujitoa mhanga maisha, vifaa vya kulipuka na vifaa vya kulipulia mabomu.

Balozi wa Eritrea katika Umoja wa Mataifa amesema kampeni ya uongo dhidi ya Eritrea haiwezi kutumika kufunika ubaya unaofanywa na serikali ya Ethiopia dhidi ya Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com