1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf asema uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvZI

BRUSSELS:

Rais wa Pakistan, Perves Musharraf , ametoa ahadi kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki na kuwa atakabithi madaraka kwa yoyote atakaeibuka mshindi.Musharraf ameyasema hayo mjini Brussels kabla ya mkutano wake na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya-Javier Solana. Ziara ya kiongozi wa Pakistan ya siku nne katika bara la Ulaya ina nia ya kuinua umaarufu wake katika nchi za magharibi.Kabla ya ziara hii, maofisa wa umoja wa Ulaya,walikuwa wameweka shinikizo kwa Musharraf la kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa wazi huku kukiwa na tetesi kuwa nchi hiyo, yenye silaha za nuklia , inaweza ikakumbwa na vurugu.Rais Musharraf anashtumiwa na wakosoaji kwa kushindwa kumpa, marehemu Benazir Bhutto, ulinzi wa kutosha.Benazir Bhutto aliwahi kuwa waziri mkuu wa Pakistan na aliuawa Novemba 27.