1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G7 walaani Korea Kaskazini kuipatia Urusi silaha

8 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Kundi la Mataifa ya Magharibi yaliyoendelea kiviwanda G7, ambao wanakutana Tokyo, Japan wamelaani vitendo vya Korea Kaskazini kuendelea na majaribio ya makombora na kuipatia silaha Urusi.

https://p.dw.com/p/4YYNf
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa matifa ya G7 ukiendelea wakati waziri wa mambo ya Nje Ukraine Dmytro Kuleba akifatilia mkutano kwa njia ya video.
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa matifa ya G7 ukiendelea wakati waziri wa mambo ya Nje Ukraine Dmytro Kuleba akifatilia mkutano kwa njia ya video.Picha: Tomohiro Ohsumi/AP Photo

Wizara ya mambo ya nje ya Japan imesema vitendo hivyo vya Korea Kaskazini vinakiuka moja kwa moja maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Shirika la kijasusi la Korea Kusini limebaini kuwa jirani yake imeipa Urusi zaidi ya makombora milioni moja yanayotumiwa katika vita vyake nchini Ukraine.

Mawaziri hao wa masuala ya kigeni wa G7 wametoa msimamo wa pamoja kuhusu vita vya Mashariki ya Kati, huku wakiilani Hamas na kusema Israel ina haki ya kujilinda, lakini wakatoa wito wa kusitishwa kwa muda mapigano ili kuharakisha msaada wa kibinaadamu katika ukanda wa Gaza.

Soma pia:Mataifa ya Magharibi yanajibu gani kuhusu Korea kaskazini kupanda

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka Israel kutoikalia tena Gaza mara tu vita vyake na Hamas vitakapomalizika. Viongozi hao G7 watajadili pia mikakati ya kukabiliana na ushawishi unazidi kuimarika wa China, pamoja na mahusiano na mataifa ya Asia ya Kati.