1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Marekani, Korea Kusini, Japan kufanya mazoezi ya kijeshi

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Korea Kusini, Marekani na Japan zitafanya luteka za pamoja za kijeshi Jumapili ijayo zitakazoishirikisha ndege ya Marekani yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia chapa B-52.

https://p.dw.com/p/4XfjH
Chinesischer Kampfjet
Ndege za China kwenye mafunzo ya kijeshi.Picha: CCTV/AP/picture alliance

Ndege hiyo iliwasili Korea Kusini siku ya Jumanne.

Duru ya jeshi ambayo haikutajwa imeliambia shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap kwamba mazoezi hayo yatakuwa ya kwanza ya aina yake kuwahi kufanywa karibu na eneo la Korea.

Soma zaidi: Korea Kaskazini yajiandaa na majaribio ya makombora

Afisa katika wizara ya ulinzi ya Korea Kusini amekataa kuthibitisha ripoti hizo lakini akasema nchi hizo tatu zinatanua luteka za pamoja kukabiliana na kitisho cha nyuklia na mashambulizi ya makombra kutoka Korea Kaskazini.