1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini, Marekani, Japan wafanya luteka la pamoja

Amina Mjahid
22 Oktoba 2023

Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya luteka ya pamoja ya kijeshi leo Jumapili, kwa mujibu wa jeshi la Seoul.

https://p.dw.com/p/4XsNc
Südkorea | USS Ronald Reagan
Meli ya kivita ya Marekani, USS Ronald Reagan, ikiwa kwenye bandari ya Busan, Korea Kusini.Picha: Kang Duck-chul/Yonhap/AP/picture alliance

Zoezi hilo lililohusisha ndege ya Marekani yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia aina ya B-52 linakuja wakati mataifa hayo matatu yakiunganisha nguvu zake kukabiliana na kitisho cha nyuklia na mashambulizi ya makombora kutoka Korea Kaskazini. 

Ndege hiyo ya Marekani iliwasili Korea Kusini siku ya Jumanne.

Soma zaidi: Lavrov aikosowa "sera ya hatari" ya Marekani kwa Korea Kaskazini

Hata hivyo, Korea Kaskazini inaliona zoezi hilo kama majaribio ya kuivamia nchi yake na imetoa onyo la mara kwa mara kwamba itachukua hatua ya kujibu zoezi hilo inaloliita la kichokozi.