1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lavrov aikosowa "sera ya hatari" ya Marekani

19 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameikosoa Marekani pamoja na washirika wake, Japan na Korea Kusini, kwa kuendeleza kile alichokiita "sera hatari ya kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini."

https://p.dw.com/p/4XjnX
Russland Moskau | Russischer Außenminister | Sergei Lavrov
Picha: Sergei Ilnitsky/REUTERS

Lavrov aliyasema hayo alipowasili na kufanya mazungumzo na maafisa wa  Pyongyang siku ya Alkhamis (Oktoba 19), akiongeza kuwa ana wasiwasi wa kuongezeka kwa shughuli za kijeshi za Marekani na washirika wake katika ukanda huo.

"Tunapinga hatua hiyo isiyojenga na iliyo ya hatari." Alisema Lavrov.

Soma zaidi: Jumuiya ya ASEAN yahofia mizozo mipya

Aidha mwanadiplomasia huyo mkuu wa Urusi alisema nchi yake inaunga mkono "mchakato wa mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu masuala ya usalama, katika Rasi ya Korea".

Lavrov alisema Moscow, Beijing na Pyongyang zinataka kupendekeza "njia mbadala" ili kupunguza mivutano katika eneo hilo.

Mikutano ya Lavrov mjini Pyongyang inatarajiwa kuweka msingi wa ziara ya baadaye ya kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin.