1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANAGUA:Ortega aapishwa kuongoza Nicaragua nakusema anachana na uhafidhina wa itikadi za kisoshalisti

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbw

Mfuasi wa zamani wa siasa za kimaxi, na aliyekuwa hasimu wa Marekani wakati wa enzi ya vita baridi, Daniel Ortega ameapishwa kuwa Rais wa Nicaragua miaka 17 baada ya kuondolewa kwa kura katika nafasi hiyo.

Daniel Ortega mwenye umri wa miaka 61 ambaye alishinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka jana amesema kuwa atapambana na umasiki nchini humo.

Amesema kuwa anaachana na siasa za itikadi kali na kwamba anataka kuwa na uhusiano mzuri na Marekani.Hata hivyo rafiki yake mkubwa ni Hugo Chavez Rais wa Venezuela ambaye ni hasimu wa Rais Bush wa Marekani.Venezuela imekuwa ikiisaidia Nicaragua kiuchumi.

Daniel Ortega aliingia madarakani mwaka 1979 katika mapinduzi yaliyomuondoa madarakani dikteta Anastazio Somoza.Lakini alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 1990.

Nchini Venezuela Rais Hugo Chavez ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha tatu cha miaka sita.

Chavez amesema kuwa atatumia kipindi hiki kuibadilisha Venezuela kuwa taifa la itikadi kali za kisoshalisti.

Tayari ametangaza mipango ya kutaifisha makubwa makubwa mawili ya umeme na mawasiliano.