1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maisha ya raia yahifadhiwe nchini Afghanistan anasema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBmz

Berlin:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier,akihojiwa na Radio Deutsche Welle,ameahidi jukumu la wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistamn litatathminiwa upya.“Bunge la shirikisho Bundestag litakapopiga kura tena msimu wa mapukutiko ujao kuamua kama shughuli za jeshi la shirikisho Bundeswehr zirefushwe,litazushwa pia suala wapi shughuli hizo ziendelezwe.Kuna haja ya kuepukana na „dhana wanajeshi wa Ujerumani wanataka kuivamia Afghanistan“ amesema waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinemeier kupitia Radio Deutsche-Welle aliyehimiza maisha ya raia wa kawaida yahifadhiwe katika harakati zote za kijeshi.