1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Ujerumani na Iran

Oumilkher Hamidou18 Juni 2009

Wanafunzi wateremka majiani nchini Ujerumani

https://p.dw.com/p/ISlJ
Kitambulisho cha maandamano ya wanafunzi ColognePicha: picture-alliance/ dpa

Mandamano ndio mada iliyohanikiza magazetini hii leo:Maandamano ya wanafrunzi nchini Ujerumani na maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi nchini Iran.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINER ZEITUNG limeyatumia maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu na wa shule za sekondari kukosoa mageuzi ya mfumo wa elimu nchini Ujerumani.Gazeti linaandika:

"Kosa kubwa kabisa ni ile hali kwamba vyuo vikuu vimepitishiwa mageuzi ya kina bila ya kupatiwa njia zinazohitajika kuyatekeleza.Baadhi ya malengo mtu anaweza kusema hayana maana yoyote:kupunguzwa muda wa masomo na wakati huo huo kuzidi kishindo cha maafunzo hakuwarahisishii mambo wanafunzi .Kwamba tena vyuo vikuu vinalazimika kuwachukua wanafunzi wengi zaidi bila ya kuwa na idadi inayohitajika ya wahadhiri,hali hiyo nayo pia inazidi kukorofisha mambo.Tangu muda sasa waziri wa elimu wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Anette Schavan amekua akizungumzia juu ya umuhimu wa kujiambatanisha na wakati katika kutia njiani mageuzi .Wakati umewadia sasa ,maneno hayo kutekelezwa kivitendo."

Gazeti la MÜNCHNER MERKUR linahisi:

"Elimu haijaandaliwa kwa misingi ya haki kijamii.Hali hiyo inaanzia katika shule za chekechea ambako CSU na FDP wamekua wakichelewesha uamuzi wa kuondowa malipo na kumalizikia katika ada za chuo kikuu.Ni mtihani mkubwa huo kwa wanafunzi ikiwa hawana mtu wa kuwasaidia.Mgogoro wa fedha unaitikisa elimu-hakuna la ziada."

Gazeti la NEUE PRESSE la mjini Hannover linauangalia mzozo juumla kama ifuatavyo:

"Cha kusikitisha zaidi ni ule ukweli kwamba kizazi kizima kinachochipuka na kuelimika vya kutosha,hakina nafasi ya kupata kazi kwasababu ya mgogoro wa kiuchumi na fedha.Shahada ya Abitur,masomo ya chuo kikuu,kuendelea na masomo nchi za nje,mazoezi ya kazi hayasaidii kitu,ukosefu ajira-hiyo ndio picha inayotawala vichwani mwa watu.Na pengine sura hiyo ya kutisha ndio inayowafanya vijana wateremke majiani."

Mada yetu ya pili inahusiana na hali ya mambo nchini Iran.Gazeti la MAGDEBURGER VOLKSSTIMME linahisi hali hiyo haikadiriki:Gazeti linaendelea kuandika:


Iran Wahlen Reaktionen Demonstration Mir Hossein Mussawi Anhänger in Teheran
Wafuasi wa Mussawi waandamana TeheranPicha: AP

"Hata kama maandamano yataleta tija na mgombea wa upande wa upinzani Mussavi kuingia madarakani,kipi kitabadilika ?Watu wategemee nini kutoka kwake? Yeye mwenyewe si miongoni mwa wenye kutawala!Picha kama hiyo iko mbali kugeuka ukweli wa mamvbo,hata hivyo watawala wanajikuta wakibanwa kila upande-ushahidi ni huu wa kupigwa marufuku ripoti zisitolewe.Marufuku hayo lakini hayazingatiiwi,watu wanatumia mtandao ,kupitia tovuti kwa mfano ya Twitter.Serikali inaonyesha kupitwa na wakati."

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linatilia mkazo umuhimu wa njia mpya ya mawasiliano katika kuwapasha watu habari.Gazeti linaendelea kuandika:

"Kishindo kikubwa kinashuhudiwa nchini Iran.Yeyote anaejitahidi kufuatilizia matokeo kupitia mtandao wa Internet,anatambua umuhimu wa vyombo vya habari vya jamii katika hali kama hiyo ya mzozo.Maandamano ya umma ya yamejipatia uwanja mpana kabisa kupitia maoni ya umma au Blog, mtandao na tovuti kama vile Facebook,Twitter na magazeti ya kimataifa,Radio na televisheni yanayoonyesha moja kwa moja jinsi serikali inavyojaribu kuwakandamiza wapinzani."

Mwandishi :Oummilkheir Hamidou /DT Zeitungen

Mhariri:M. Abdul-rahman