1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Blair azitetea juhudi za kijeshi za Uingereza nchini Afghanistan na Irak

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbL

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameitetea nchi yake kwa kujihusisha kijeshi nchini Afghanistan na Irak akisema diplomasia pekee haiwezi kutatua matatizo yanayoikabili dunia.

Katika hotuba yake aliyoitoa mjini Plymouth, Blair amesema diplomasia inatakiwa kufuatiwa na harakati ya kijeshi kuzuia ugaidi. Hata hivyo waziri Blair amekiri juhudi za Uingereza nchini Afghanistan na Irak zinalilemea jeshi la Uingereza.

Amesema bajeti ya jeshi itabidi iongoezeke kama sera yake ya kujiingiza kijeshi itaendelezwa. Blair ameyasema hayo siku moja baada ya rais George Bush wa Marekani kutangaza mpango wa kutaka kuongeza wanajeshi zaidi nchini Irak.