1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Serikali na waasi waongeza muda wa suluhu

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCil

Serikali ya Uganda na waasi wa LRA wameongeza muda wa suluhu hadi mwishoni mwa mwezi wa Februari mwakani.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalianza tena hapo Alhamisi katika mji wa kaskazini mwa Sudan wa Juba ikiwa ni wiki tatu baada ya LRA kujitowa kwenye mazungumzo hayo kwa kulishutumu jeshi la Uganda kwa kuwashambulia wapiganaji wake na kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliofikiwa hapo mwezi wa Augusti.

Licha ya kuwepo kwa hali ya kutoaminiana na kushutumiana kwa ukiukaji wa suluhu hiyo kutoka pande zote mbili usitishaji huo wa mapigano kwa kiasi kikubwa umeweza kudumu na kuleta matumaini ya kumalizika kwa vita vya miaka 20 vya wenyewe kwa wenyewe ambako kutaruhusu kurudi nyumbani kwa wakimbizi milioni moja na laki nne.

Usitishaji huo wa mapigano unavitaka vikosi vya LRA kukusanyika kwenye sehemu mbili kusini mwa Sudan wakati mazungumzo hayo yakiendelea.