Juhudi za rais john Kofour za upatanishi zitafaulu Kenya? | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 10.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Juhudi za rais john Kofour za upatanishi zitafaulu Kenya?

---

NAIROBI

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na mpatanishi katika mzozo wa kisiasa nchini Kenya rais wa ghana John Kufour ilimlazimu kurefura kwa siku moja ziara yake nchini humo ili kujaribu kuutatua mvutano wa kisiasa uliopo katika taifa hilo la Afrika mashariki.Mvutano huo ulisababishwa na matokeo ya urais yanayotiliwa shaka ambapo rais Kibaki alipata ushindi dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga ambaye anasema Kibaki aliiba Kura.Hapo jana rais Kofour alikutana tofauti na Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga.Hata hivyo mazungumzo hayo hayakufanikiwa kutokana na pande zote mbili kushikilia misimamo yao.Chama cha ODM cha bwana Raila kinasema katu hakitamtambua Kibaki kama Rais wala serikali yake huku upande wa bwana Kibaki ukishikilia kwamba ulichaguliwa kihalali na hivyo utaendelea kuwa serikalini.Matokeo ya uchaguzi war ais yalikosolewa na waangalizi wote wa kimataifa pamoja na wakenya.Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikitoa mwito kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya kutafuta njia za kuleta maridhiano ili kuleta utulivu.Ghasia za siku kadhaa nchini humo zilisababisha watu zaidi ya 500 kuuwawa na maelfu wakiendelea kuishi kwenye makambi wakihofia kuvamiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com