1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali bado tete nchini Kirgistan

Sekione Kitojo19 Juni 2010

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa , Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa wanachama wa umoja huo kuchangia misaada ya kiasi cha euro milioni 58 kwa ajili ya nchi ya Kirgistan.

https://p.dw.com/p/NxEl
Waandamanaji wanajikusanya mbele ya jengo la serikali wakizuiwa na polisi katika mji wa Talas, nchini Kyrgyzstan.Picha: AP

NEW YORK:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa mwito kwa wanachama wa umoja huo kuchanga msaada wa kiasi cha Euro milioni 58 kwa ajili ya nchi ya Kyrgyzstan iliyokumbwa na machafuko ya kikabila. Ban ki-moon amesema fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia kiasi ya wakimbizi 300,000 na raia wengine walioathirika kwa machafuko hayo.

Hapo awali,Rais wa mpito wa Kyrgyzstan, Rosa Otubajewa alikiri kuwa idadi ya watu waliouawa huenda ikawa ni 2,000 - hiyo ni mara kumi zaidi ya vile ilivyotathminiwa hapo awali. Wakati huo huo Urusi inafikiria kupeleka wanajeshi wake nchini Kyrgyzstan ili kulinda vituo muhimu nchini humo. Lakini uamuzi bado haujapitishwa. Hiyo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi vilivyoinukulu wizara ya ulinzi mjini Moscow.