1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Haki za wavumiliwa kuweza kuishi Ujerumani

Hiyo ndio mada kuu iliohaririwa na magazeti ya leo ya Ujerumani.hii inafuatia muafaka kati ya vyama-tawala juu ya hali za watu wa aina hii wasioweza kufanya kazi hata wakizipata.

Wakati vyama-tawala vya CDU/CSU na washirika wao serikalini SPD wanashangiria maafikiano hayo, Upinzani unakosoa ukidai wakaazi hao wakigeni hawakutendewa inavyostahiki hasa.

Gazeti la BERLINER ZEITUNG linaona kwamba walioshinda katika mvutano huu, ni wale wenye siasa kali katika vyama vya CDU/CSU ambao azma yao ni kuwatisha raia wa kigeni wasihamie Ujerumani.Katika kila hatua ya kuwahurumia, wao huona hiyo ni kuwatia shime watakao kuhamia Ujerumani.Wala hawaoni haya kupiga upatu na kuhanikiza biramu lao kuwa wageni hao wanaishi humu nchini kwa jasho la wajerumani.

Jinsi gani siasa ya nje ya Ujerumani ni mfungwa wa siasa za kujitenga na wageni, ushahidi ni lugha inayotumiwa:Mwanasiasa wa vyama vya CDU/CSU asema ruhusa ya kuwavumilia wageni hao kuishi nchini kwa majaribio tu itolewe hadi 2009.hii ina maana mgeni huyo licha ya kuwa ameshaishi humu nchini miaka mingi,licha ya kubidi kuthibitisha uwezo wake wa kuzungumza kijerumani,hakufanya hatia yoyote,anabidi pia kuhetimu mitihani ya kuishi Ujerumani.”

Ama Frankfurter Allgemeine Zeitung laandika:

“Serikali za mikoa ambazo zilijitutumua hadi mwisho kuzuwia kuregezwa masharti ya kuondolewa nchini kwa wageni wa aina hii,inabidi sasa kuachana na ndoto zao kwamba yawezekana kufanya masharti ya kuwavumilia wageni kubakia nchini si mazuri hadi mwenyewe waamue binafsi kufunga virago na kuondoka nchini.

Mbinu hii haikufanya kazi kwavile wakaazi wengi wanaovumiliwa tu kubaki nchini,hawana njia nyingi nyengine za kuwavutia kuihama nchi hii.Kwa kuwakomea mlango wa soko la kazi watu hawa matokeo yake ni kinyume na ilivyotarajiwa:Wanahamia kuuhujumu mfuko wa malipo ya ruzuku humu nchini.”

Gazeti la Stuttgarter zeitung katika muafaka uliofikiwa na vyama tawala, linaona kuna manufaa nadhara:Laandika:

“Haki mpya ya kuishi nchini kwa wageni wanaovumiliwa inakomesha mjadala wa miaka mingi usio na faida yoyote.Na hii pekee ni maendeleo.Kwani, mwishoe, kinachohesabika ni kwamba serikali ya shirikisho na za mikoa ziliweza alao kuafikiana juu ya ufumbuzi wa kitandawili hiki.Muafaka huo usingewezekana na mshirika mwengine serikalini mbali na SPD.Umenunuliwa kwa mhanga mkubwa.

Kwani chama cha SPD (kinachowatetea wanyonge) sio tu kimebidi kuridhia hatari funali kwa wanyoge hao bali pia kimebebea dhamana zaidi za kukazwa zaidi masharti ya sheria zinazowabana wageni.Kwani, gharama walipao ni wale wanaohamia nchini.Kwa wakimbizi ,Ujerumani zamani imeshageuka nchi isiokaribisha wakimbizi.”

Gazeti la HESSISCHE/NIEDERSÄCHSISCHE ALLGEMEINE kutoka Kassel linamurika hali ya kutatanisha wanayojikuta wagerni wengi waishio humu nchini:

Hadi sasa,laandika gazeti, wageni waliovumiliwa tu kubakia nchini hawakuruhusiwa kufanya kazi na kwahivyo hawakuwa na njia nyengine ya kufanya kujipatia kibarua.

Sasa endapo wakitoa ushahidi wamepata kazi,ndipo wataweza kupatiwa ruhusa ya kubakia nchini.Hali hii ya kutatanisha wanayojikuta itaongoza kukubali kufanya kazi kwa masharti yoyote yale watakayopewa na waajiri.”