1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Hali ya usalama duniani inazidi kuwa mbaya

27 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema makundi ya wapiganaji katika mataifa kama vile Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo, Myanmar, Ukraine, Sudan na Ukanda wa Gaza yanapuuza sheria za kimataifa.

https://p.dw.com/p/4cv43
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Karim Jaafar/AFP/Getty Images

Antonio Guterres ametoa wito kwa viongozi kujitolea kwa ajili ya amani na usalama duniani kote na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.

Akizungumza wakati wa kikao chake cha kwanza cha baraza la haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Katibu Mkuu huyo ametahadharisha kuwa hali ya usalama inazidi kuwa mbaya duniani.

Ameongeza kuwa, mizozo duniani inawasababishia watu mateso makubwa na haki zao binadamu kutoheshimiwa.

Soma pia: Guterres atahadharisha dhidi ya kuishambulia Rafah 

Guterres pia amelitetea shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, akilitaja kama uti wa mgongo kwa juhudi za usaidizi katika ukanda wa Gaza wakati linakabiliwa na shinikizo la kutaka kuvunjwa.

"Moja ya ahadi ya ulinzi ya mashirika yote ya Umoja wa Mataifa ni kufanya kila linalowezekana kulinda watu."

Naye Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ametahadharisha kuwa kazi ya chombo hicho iko hatarini kutokana na kile alichokiita kuwa "majaribio ya kuendelea kudhoofisha uhalali na kazi ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine".