1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GENEVA.Maafisa wa umoja wa mataifa wanyimwa visa za kuingia Sudan

Maafisa wa haki za kibinadamu wa umoja wa mataifa wamevunja safari yao ya kuelekea katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan baada ya serikali ya Khartoum kuwanyima visa za kuingia nchini humo.

Msemaji wa kikosi hicho cha maafisa wa umoja wa mataifa amesema kuwa kundi lake sasa litalazimika kukusanya habari juu ya mateso dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur kutoka nje ya Sudan.

Maafisa hao walikuwa wakisubiri kupewa visa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema kuwa haitawaruhusu watetezi hao wa haki za binadamu kuingia Khartoum iwapo hawatamtoa katika kundi lao afisa mmoja ambae Sudan imemtaja kuwa ni adui.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com