FREETOWN: Hali ya wasiwasi yatanda huku matokeo ya uchaguzi yakisubiriwa
14 Agosti 2007Matangazo
Polisi nchini Sierra Leone iko katika hali ya tahadhari kabla matokeo ya mwisho ya uchaguzi kutolewa.
Hali ya wasiwasi imetanda nchini humo baada ya matokeo ya awali kuonyesha kuwa chama cha upinzani cha All People´s Congress, APC, kinaongoza na upinzani umewatolea mwito wafuasi wake wajitokeze barabarani kusherehekea ushindi.
Rais Ahmad Tejan Kabbah ameviamuru vikosi vya usalama viwe katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na machafuko yoyote yatakayotokea.