Frankfurt, Ujerumani. Siemens yateua mtendaji mkuu mpya. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Frankfurt, Ujerumani. Siemens yateua mtendaji mkuu mpya.

Bodi ya utendaji ya kampuni ya vyombo vya elekroniki ya Siemens imemtea mkurugenzi mpya mtendaji.

Peter Löscher, ambaye kwa hivi sasa ni meneja mwandamizi wa kampuni la utengenezaji wa madawa nchini Marekani la Merck, atachukua nafasi ya afisa mkuu mtendaji anayeondoka madarakani Klaus Kleinfeld ifikapo Julai mosi.

Kampuni la Siemens limekabiliwa katika miezi ya hivi karibuni na madai kuwa ililipa mamilioni ya Euro kama hongo ili kupata mikataba minono ya nje.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com