COPENHAGEN : Ujerumani na Danmark kujenga daraja | Habari za Ulimwengu | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COPENHAGEN : Ujerumani na Danmark kujenga daraja

Ujerumani na Denmark zimekubaliana kujenga mojawapo ya madaraja makubwa kabisa kupitia Bahari ya Baltiki.

Daraja hilo la kilomita 19 litavuka Ukanda wa Fehmarn na kupunguza masaa ya usafiri kwa nusu kutoka mji wa Hamburg nchini Ujerumani hadi katika mji mkuu wa Denmark Copenhagen.

Vyombo vya habari vya Danmark vimesema ujenzi wa mradi huo wa euro bilioni tano na nusu utaanza hapo mwaka 2011 na kumalizika mwaka 2018.

Uamuzi wa kujenga daraja hilo ni pigo kwa shirika la Scandilines ambapo vivuko vyake hufanya kazi kwa masaa 24 kwa siku kwenye njia hiyo ya bahari.

Ujenzi wa daraja hilo yumkini pia ukakabiliwa na upinzani kutoka kwa wanamazingira.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com