1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CEBU: Mataifa ya Kusini Mashiriki mwa Eshia yaidhinisha mkataba wa kupambana na ugaidi.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaw

Viongozi wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Eshia wametia saini mwafaka wa kupambana na ugaidi.

Kwenye mkutano wao wa kila mwaka katika kisiwa cha Cebu nchini Philippines, viongozi hao wa Umoja wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Eshia waliafikiana kuwa na mkataba huo ambao ni wa kwanza kuhusu ugaidi kuwahi kutiwa saini katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mkataba huo, mataifa hayo yanatakiwa yaimarishe ushirikiano wao kudhibiti ugaidi na yashirikiane kupeleleza matukio ya ugaidi.

Mataifa yote kumi wanachama wa Umoja huo pia yamekubaliana kuwa na eneo la biashara huru kufikia mwaka elfu mbili na kumi na tano.

Kikao hicho kiliahirishwa mwezi Disemba baada ya mataifa kadhaa ikiwemo Marekani, Australia, na Uingereza kutahadharisha uwezekano wa kutukia shambulio la kigaidi.

Umoja huo unajumuisha Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Burma, Philippines, Singapore, Thailand na Vietnam.