BRUSSELS:Urusi bado yathamini uhusiano wake na Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS:Urusi bado yathamini uhusiano wake na Uingereza

Balozi wa Urusi nchini Uingereza Yuri Fedotov anashikilia kuwa nchi yake bado inathamini uhusiano wake na Uingereza.katika barua yake iliyochapishwa kwenye gazeti la The Times la hii leo,balozi huyo anakanusha tena madai kuwa Urusi ilihusika na mauaji ya afisa wa ujasusi wa zamani Alexander Litvinenko.Mauaji hayo yalitokea mjini London mwaka jana.Urusi bado haijatoa tamko lake rasmi baada ya Uingereza kuwakufukuza wanadiplomasia wake wanne mwanzoni mwa wiki hii baada ya kukataa kumrejesha mshukiwa mkuu wa mauaji hayo Alexander Lugovoi kushtakiwa.Uingereza imelaumiwa na wanasiasa kadhaa wa Urusi kwa kukataa kumrejesha nchini mwake Boris Berezovsky ,mfanyibiashara mkubwa na mjumbe wa serikali ya utawala wa wachache ili kushtakiwa.Bwana Berezovsky anadai kuwa kuna njama ya kumuua iliyopangwa na serikali ya Rais Putin.Aliyasema hayo katika mahojiano na BBC.

''Ni muhimu kuelewa kwamba baada ya kifo cha Litvinenko mataifa ya magharibi yajue hasa Putin ni nani kwani ni mhalifu na anafanya anavyotaka yeye.Si kitu kigumu kuelewa.''

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com