BERLIN :Ujerumani na Urusi kujadilia ushirikiano na suala la makombora ya kujihami | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN :Ujerumani na Urusi kujadilia ushirikiano na suala la makombora ya kujihami

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anasisitiza umuhimu wa kushirikiana na Urusi katika masuala ya kimataifa huku akijiandaa kwa mkutano na Rais wa Urusi Vladimir Putin hii leo mjini Wiesbaden.Bi Merkel anatarajiwa kukutana na Rais Putin pembezoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya Urusi na Ujerumani kwa jina Petersburg Dialogue.Kikao hicho kilianzishwa na Kansela wa Ujerumani wa zamani Gerhard Schroeder mwaka 2001.

Viongozi hao wanapanga kujadilia suala la Iran,mustakabal wa jimbo la Kosovo huku Urusi ikiongeza kuwa itazungumzia mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya Mashariki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com