1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani kupata ziada kutokana na ukuaji wa uchumi.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4l

Ukuaji wa uchumi nchini Ujerumani unaweza kuipatia nchi hiyo ziada ya kiasi cha Euro bilioni 90 kutokana na mapato ya kodi katika muda wa miaka minne ijayo.

Waziri wa fedha Peer Steinbrück ameliambia gazeti la Welt am Sonntag, lakini amesema hata hivyo kuwa hiyo isiwe sababu ya kushangilia sana.

Matumizi ya umma kwa ajili ya bima ya afya , gharama za kazi na punguzo la kodi ya makampuni itafikia kiasi cha Euro bilioni 50.

Taasisi ya IFW yenye makao yake katika mji wa Kiel, moja kati ya taasisi muhimu za ushauri wa kiuchumi nchini humo , hivi karibuni iliopandisha makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi wa Ujerumani mwaka huu na mwaka ujao kwa kuangalia kile inachosema kuwa ni mapato makubwa katika mahitaji ya ndani pamoja na mahitaji kamili ya bidhaa nchi za nje.