Baraza la usalama la Umoja wa mataifa lalaani hali ya Darfour | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa lalaani hali ya Darfour

New-York:

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limeelezea wasi wasi wake kutokana na njama za makundi ya waasi wanaotaka kuipundua serikali ya Tchad na ku hali inavyozidi kua mbaya Darfour.Mwenyekiti wa taasisi hiyo muhimu ya Umoja wa mataifa,Nasser Abdelaziz wa Qatar amesema,baraza la usalama linalaani njama za kutaka kuvuruga hali nchini Tchad.Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeelezea pia hofu kuelekea hali inayozidi kua mbaya Darfour.”Ufumbuzi wa amani wa mzozo wa Darfour utachangia kurejesha usalama na utulivu katika eneo hilo,na hasa nchini Tchad na katika jamhuri ya afrika kati-limesema baraza la usalama kabla ya kusisitiza umuhimu wa kuheshimiwa uhuru na milki ya nchi zote za eneo hilo.”

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com